Habari Mseto

Benki ya Equity pia yapata faida

August 16th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU
Benki ya Equity imetangaza faida ya asilimia 18 baada ya kutozwa ushuru kwa miezi sita ya mwanzo 2018.

Benki hiyo Alhamisi ilitangaza faida hiyo na kusema kuwa ilitokana na mapato yanayotokana na riba na hatua za usimamizi zilizozinduliwa.

Faida yake iliongezeka hadi Sh11 bilioni kutoka Sh9.4 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka wa 2017.

Mapato kutokana na riba yalipanda kwa asilimia tisa hadi Sh19.6 bilioni kutoka Sh17.9 bilioni katika kipindi hicho.

Mikopo kwa wateja iliongezeka kwa asilimia nne hadi Sh275 bilioni kutoka Sh265.1 bilioni.

Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Equity Bw James Mwangi, ongezeko hilo lilitokana na hatua ya benki hiyo ya kupanua mikondo ya mapato.