• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
CORONA: Hofu katika kambi ya wanajeshi Lanet

CORONA: Hofu katika kambi ya wanajeshi Lanet

NA RICHARD MAOSI

Kumetanda hofu katika mtaa wa Umoja Lanet baada ya lori kusafirisha idadi ya watu wasiojulikana kutoka kweye makazi ya kifahari hadi kwenye karantini ya lazima.

Hii ni baada ya waziri wa afya Mutahi Kagwe siku ya Alhamisi kutangaza kisa cha mwathiriwa wa Covid-19 kutoka Nakuru, ambapo hatimaye ilibainika alikuwa ni mwanadada kutoka kaunti ya Mombasa.

Mwanadada huyo alizuru Lanet tarehe 27 Machi, ambapo amekuwa akiishi na dadake pamoja na mumewe ambaye ni afisa wa jeshi kutoka Lanet Barracks.

Ingawa haijulikani mwanadada alikuwa ametangamana na watu wangapi, ilibidi ploti nzima kusombwa na lori ili kutumikia kuarantini ya lazima, huku uchunguzi wa kina ukiendelea ili kutathmini idadi ya watu ambao huenda walikuwa wameambukizwa bila kujua.

Duru za kuaminika zilidokezea Taifa Leo Dijitali kuwa afisa huyo wa jeshi alikuwa kazini na amekuwa akitangamana na wenzake wakati wa kazi.

Aidha jambo hili lilisababisha kambi ya Lanet kufungwa kwa wiki mbili huku shughuli zote zikisitishwa kutadhmini wale ambao huenda walikuwa washirika wa karibu wa afisa huyo.

Juhudi za Taifa Leo Dijitali kuzungumza na Colonel Paul Njuguna kwa njia ya simu ziligonga mwamba kwani hakupokea simu wala kujibu arafa zetu.

Aidha Kariuki Gichuki ambaye ni mkurugenzi wa afya kutoka idara ya afya kaunti ya Nakuru alisema hakua na habari kuhusu kuarantini ya lazima, eneo la Lanet.

You can share this post!

Saburi atupwe jela miaka 10 – Uhuru

Hofu wabunge 17 wana virusi vya corona

adminleo