• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 9:50 AM
Deacons sasa kuuzwa kulipa madeni

Deacons sasa kuuzwa kulipa madeni

Na BERNARDINE MUTANU

Wasimamizi wa duka la rejareja la kuuza nguo, Deacons Afrika Mashariki, wameamua kuuza kampuni hiyo kwa lengo la kupata pesa za kulipa madeni.

Kampuni hiyo inadaiwa zaidi ya Sh1 bilioni. Katika notisi Jumanne, wasimamizi Peter Kahi na Atul Shah kutoka kampuni ya uchunguzi wa kifedha PKF waliwataka wote wanaohitaji kununua mali kutuma ombi kupitia Dyer & Blair.

Biashara zinazouzwa ni 4U2, Adidas, Bossini na FNF. Nane kati ya biashara hizo zimo Nairobi ila Bossini, ambayo imo Rwanda.

“Katika mkutano wa wakopeshaji uliofanywa Januari 22, pendekezo la wasimamizi liliidhinishwa kuuza mali kwa njia wazi kwa kuhusisha mshauri,” walisema katika notisi ya pamoja.

Ripoti ya wasimamizi hao wa Deacon iliyochapishwa mwaka jana ilionyesha kielelezo cha kampuni hiyo, ambacho kilipelekea wakopeshaji zaidi ya 120 kupata hasara kuu baada ya kusambaratika kwa mapato ya kampuni hiyo.

Mali muhimu zaidi ya Deacons ni fenicha na bidhaa, kiwango kisichoweza kuwalipa wakopeshaji wote.

Kwa karatasi, Deacons ina mali ya thamani ya Sh606 milioni, lakini kulingana na PKF, mauzo ya mali hiyo yanaweza kuipa kampuni hiyo Sh63 milioni pekee.

Kampuni hiyo ilipata hasara ya Sh558 milioni katika muda wa miezi 11 kufikia Novemba 2018.

You can share this post!

Van Persie ataka Ole Gunnar apewe muda zaidi

Aliyekuwa kocha wa Brighton asema hakutarajia angepigwa...

adminleo