Dominic Kimengich ateuliwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Eldoret
Na JEREMIAH KIPLANG’AT
PAPA Francis wa Kanisa Katoliki amemteua Dominic Kimengich kuwa Askofu wa Dayosisi ya Eldoret, wadhifa uliobaki wazi tangu kifo cha Cornelius Korir mwaka 2017.
Askofu wa muda mrefu wa Lodwar ameteuliwa Jumamosi kuongoza Dayosisi hiyo iliyokuwa ikiongozwa japo kwa ukaimu na Askofu Maurice Crowley wa Dayosisi ya Kitale tangu kittokee kifo cha Askofu Korir mnamo Oktoba 2017.
Askofu Crowley amethibitishia Taifa Leo mabadiliko hayo.
“Ni kweli Dominic Kimengich atakuwa Askofu mpya wa Dayosisi ya Eldoret,” amesema Askofu Crowley.
Kuteuliwa kwa Askofu Kimengich kunajiri takribani miaka miwili tangu ombwe kujengeka baada ya kifo cha Korir.
Atakayejaza nafasi ya Kimengich huko Lodwar anasubiriwa kubainika.
Ashofu Korir aliaga dumnia baada ya kuugua kisukari na kusumbuliwa na shinikizo la damu.
Mchango wake katika jamii ungali unakumbukwa, hasa kujitolea kwake wakati wa uhai wake kuongoza majadiliano ya amani baina ya jamii za eneo la North Rift.