Habari Mseto

Faida ya Kenya Power yaanza kuporomoka

October 23rd, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya Umeme ya Kenya Power imetoa onyo la faida. Kampuni hiyo ilionya kuwa mapato yake yatapungua kwa asilimia 25 ishara kwamba hali itakuwa ngumu sana kwa wenye hisa.

Inamaanisha kuwa faida ya kampuni hiyo katika mwaka wa kifedha kufikia Juni 2018 imeenda chini ikilinganishwa na muda kama huo 2017.

Kulingana na sheria, ikiwa kampuni inatarajia kupata hasara zaidi ya robo ikilinganishwa na mwaka wa kifedha uliotangulia.

Kampuni hiyo ilitangaza faida ya Sh7.27 bilioni baada ya ushuru katika mwaka wa kifedha uliokamilika Juni 2017.

Hii ina maana kuwa kampuni hiyo inatarajia faidi chini Sh5.46 bilioni kufikia Juni 2018.

Katika taarifa ya kampuni hiyo, ilisema onyo lilitolewa kuambatana na matokeo ya kifedha ambayo hayajachunguzwa.

Kampuni hiyo ilisema upungufu wa faida unatokana na hali mbaya ya uchumi, ukosefu wa maji ya kutengeneza kawi, kipindi kirefu cha uchaguzi na kukawizwa kwa tathmini ya ada ya matumizi ya umeme.