• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Hatimaye Gavana Lonyangapuo arudishiwa ulinzi

Hatimaye Gavana Lonyangapuo arudishiwa ulinzi

Na Oscar Kakai

GAVANA wa Kaunti ya Pokot Magharibi, Prof John Lonyangapuo amerudishiwa walinzi wake, miezi minane baada ya kupokonywa na serikali.

Ulinzi wa kibinafsi na wa nyumbani uliondolewa na serikali baada ya Gavana huyo kumwachilia mhudumu wa boda boda ambaye alikuwa ameshikwa na maafisa wa polisi eneo la Safari Park, na kuondoa vizuizi vya barabara kwenye barabara kuu ya Kapenguria-Lodwar.

Kamanda wa Polisi katika kaunti hiyo, Bw Jackson Tumwet alithibitisha kuwa ulinzi wa kibinafsi na wa nyumbani kwake gavana Lonyangapuo ulirejeshwa wiki iliyopita .

“Tumerejesha ulinzi wake kutokea Mei 26, na atachagua walinzi wake na wa nyumbani,” alisema Bw Tumwet.

Alisema uamuzi huo ulitokana na kuwa Prof Lonyangapuo ni kiongozi ambaye amechaguliwa na wananchi.

Kwa upande wake, gavana huyo alipongeza serikali kwa kumrejeshea ulinzi, japo miezi minane baadaye.

Baada ya tukio la kuachilia mhudumu wa boda boda, Gavana huyo alienda mafichoni maafisa wa usalama walipotaka kumshika.

Hata hivyo kupitia kwa wakili wake Peter Wanyama, Prof Lonyangapuo aliwasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Kitale kuzuia polisi kumkamata. Jaji Hillary Chemitei aliagiza asikamatwe.

Mahakama hiyo pia ilipeana Gavana huyo bondi ya kutarajiwa kukamatwa ya Sh200,000 kusimamia kushikwa kwa gavana huyo.

Jaji huyo alitoa agizo kurejeshwa kwa usalama wa Gavana huyo lakini serikali ikakaidi amri hiyo.

You can share this post!

Kongamano la walimu lainua biashara baada ya Ramadhan

Baba Yao atumia Sh6m kuwatibu wanabodaboda waliopata ajali

adminleo