• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Historia Uhuru kuandamana na mlinzi wa kike

Historia Uhuru kuandamana na mlinzi wa kike

 Na PETER MBURU

RAIS Uhuru Kenyatta ameweka historia nchini, baada ya kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hili kutumia huduma za mlinzi wa kike (ADC) tangu Kenya ilipopata uhuru.

Katika hafla ya umma kaunti ya Nyeri Ijumaa, Rais Kenyatta alitokea na mlinzi wa kike, jambo lililoibua mjadala baada ya kisa hicho cha wakati alipokuwa katika makao ya kitaifa ya Sagana State Lodge kushuhudia tamasha za muziki za shule.

Rais alikuwa mcheshi huku nyuma yake akiketi mwanamke huyo aliyevalia sare za mlinzi.

Baadaye, ujumbe kutoka ikulu Ijumaa alasiri ulisema kuwa mwanamke huyo alikuwa naibu wa ADC wa sasa Lt Col Timothy Lekolool na kuwa watakuwa wakifanya kazi pamoja.

“Rais Kenyatta kwenye mashindano ya kitaifa ya muziki. Kazini ni naibu mpya wa mlinzi wake (ADC) Lt Col Nduta Kamui wa kutoka wanajeshi wa angani ambaye atakuwa akifanya kazi pamoja na Lt Col Timothy Lekolool,” ikasema taarifa hiyo.

Bi Kamui amechukua nafasi hiyo muhimu wiki chache baada ya Rais Kenyatta kumteua Bi Fatuma Ahmed kuwa mwanamke wa kwanza kupata cheo cha Meja Jenerali nchini.

Maj Gen Bi Ahmed aliteuliwa mnamo Julai 13, wakati alipofanywa Naibu Mkuu wa majeshi ya humu nchini.

You can share this post!

Vivo Energy yapunguza bei ya mafuta kwa Sh13

Akanusha mashtaka ya kuiba mamilioni

adminleo