Habari Mseto

Jinsi mahakama ya Afrika inavyoshughulikia kesi zinazohusu haki za watu na za binadamu kwa jumla

November 22nd, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MAGDALENE WANJA

MAHAKAMA ya Afrika Inayoshughulikia Haki za Kibinadamu na Watu ilitarajiwa Alhamisi kutoa uamuzi wa kesi nane muhimu baada ya kikao cha majuma manne cha 55th Ordinary Session Visiwani Zanzibar.

Mahakama hiyo inajumuisha majaji 11 ambao wanatoka kwa nchi ambazo ni wanachama wa Muungano wa Afrika (AU) ambao wamechaguliwa kivyao.

Sita ya kesi hizo ni za nchi ya Tanzania ambapo watu binafsi wameishtaki nchi hiyo kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Katika mojawapo ya kesi, Andrew Ambrose Cheusi ambaye alifungwa kwa miaka 30 kufuatia mashtaka ya wizi wa kimabavu, anadai kuwa kifungo chake hakikufuata sheria kwani alihukumiwa chini ya sheria ambazo hazikuwepo wakati alituhumiwa kufanya makosa aliyokutwa kutekeleza.

Katika kesi nyingine inayohusisha nchi ya Rwanda, waliowasilisha kesi hiyo wanadai kuwa uongozi wa nchi hiyo ulichukua paspoti zao bila kufuata sheria.

Walidai kuwa nchi hiyo ilibatilisha paspoti hizo kisiri na waligundua walipokuwa wakijisajili kuchukua visa ya Amerika.

Kesi hizo ni za mwaka 2015.