Kafyu hii iondolewe – LSK
CHAMA cha mawakili nchini (LSK) kimefika mahakamani kikitaka kuondoloewa kwa kafyu na kumtaka Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kutoa taarifa kuhusu jinsi Kenya imejitayarisha kupambana na janga la corona.
Chama hicho kinataka agizo mbadala la kuishurutisha Wizara ya Usalama wa Ndani kuongeza wakati wa kuanza kafyu kutoka saa moja usiku hadi saa nne usiku.
Kinaitaka korti pia kumlazimisha Waziri Fred Matiang’i kuchapisha mwogozo wa jinsi polisi wanapaswa kutekeleza kafyu na kuchapisha kwa gazeti linalosambazwa kote nchini.
Kupitia kwa wanasheria Wakesho Kililo na Omwanza Ombati, chama hicho kinasaka kuundwa kwa kanunuzitakazozuia polisi kutumia nguvu kupita kiasi katika kutekeleza kafyu na iwapo polisi watakiuka kanuni hizo basi Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai atalaumiwa na kushtakiwa.
LSK kinataka korti kuagiza Bw Mutyambai akome kuingilia vyombo vya habari vinavyoonyesha jinsi kafyu inavyoendelezwa, na taaluma ya unasheria kuongezewa katika orodha ya watoaji huduma muhimu.
IMETAFSIRIWA NA FAUSTINE NGILA