KANU kujifufua kwa kufungua matawi mapya kote nchini
STANLEY KIMUGE na WYCLIFF KIPSANG
CHAMA cha KANU kimetangaza kwamba kitafungua afisi zake katika kaunti zote nchini inapopanga karata zake za kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2022.
Katibu Mkuu wa Kanu Nick Salat alisema hatua hiyo ni kati ya mikakati kadhaa ya kuongeza umaarufu wa chama huku akifichua kwamba watazindua usajili wa wanachama wapya na kuandaa uchaguzi wa mashinani hivi karibuni.
“Chama kimeamua kufungua upya matawi yake kote nchini ili kujiandaa kwa uchaguzi wa mashinani na usajiliwa wa wanachama wapya,” akasema Bw Salat baada ya mkutano wa chama mjini Nakuru, hafla ambayo ilihudhuriwa na Mwenyekiti Gideon Moi.
Bw Salat pia alisema Kanu inaunga mkono salamu za maridhiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga na mapendekezo yatakayotolewa na kamati ya kujenga madaraja iliyobuniwa na wawili hao maarufu kama BBI.
Mkutano huo wa Jumamosi pia ulihudhuriwa na wawakilishi wadi 64 wa Kanu kutoka kote nchini, madiwani ambao