Habari Mseto                                                
                                            
                                        Kaunti yasifu Sacco kwa kuinua wakazi kiuchumi na kijamii
 
                                                    
                                                        PICHA | HISANI                                                    
                                                SERIKALI ya Kaunti ya Kilifi imesifu mchango wa vyama vya ushirika kwa maendeleo ya kijamii na uchumi.
Naibu Gavana, Flora Chibule alihimiza jamii kujiunga na Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (Sacco) au kuunda vipya kwa sababu manufaa yake yanaonekana.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya Imarika DT Sacco mjini Kilifi, alisema Serikali ya Kaunti imebuni mswada ambao utatoa mazingira mazuri ya biashara kwa Sacco.