Habari Mseto

KCPE: Shule ya Msingi ya Ikombe yaibuka bingwa kitaifa

November 21st, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na Bernardine Mutanu

Shule ya Msingi ya Ikombe iliyo katika Kaunti Ndogo ya Yatta, Kaunti ya Machakos ndiyo iliibuka mshindi katika Mtihani wa Kitaifa kwa Shule za Msingi (KCPE) baada ya kuwaangusha mibabe hasa wa shule za kibinafsi. 

Watahiniwa wa KCPE  katika shule hiyo ya umma walikuwa 95 na kati yao, 94 walipata maki 400 na zaidi isipokuwa mmoja aliyepata alama 399.

Shule hiyo ilikuwa na 418 alama za wastani, “Tumefurahi sana kutokana na matokeo hayo mazuri,” alisema aliyekuwa Naibu Spika wa Kaunti wa Kaunti ya Machakos, na aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Ikombe Bw Nathaniel Nganga.

Shule hiyo ni ya kutwa na bweni na ina wanafunzi takriban 500 ambao hulala shuleni na wengine karibu 100 ambao huenda nyumbani kila siku.

Mwaka 2018, shule hiyo ilikuwa moja ya shule bora zaidi nchini kwa kuwa nafasi ya 54 kati ya 100 bora na alama za wastani 389.84.