• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Kesi dhidi ya Sonko yatupwa

Kesi dhidi ya Sonko yatupwa

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu imetupilia mbali kesi ya Sh1.7bilioni dhidi ya  Gavana Mike Sonko Mbuvi kuhusu bima ya afya.

Mwakilishu wa wadi ya Makongeni Peter Imwatok alikuwa amemshtaki Sonko akisema hatua ya kulipa kampuini ya bima ya Afya ya AAR ni ufujaji wa pesa za uma.

Lakini Jaji Hedwiq Ong’undi aliombwa na wakili Wilfred Nyamu atupilie kesi hiyo kwa vile mahakama haina mamlaka ya kusikiza na kuamua kesi hiyo.

Mahakama ilikubaliana na wakili Nyamu na kusema “ haina mamlaka kuiamua kwa vile ingelipelekwa kwa jopo inayoamua madai ya kunyimwa kandarasi.”

Jaji Ong’udi alisema mlalamishi angepeleka madai yake kwa tume ya kupambana na ufisadi EACC.

You can share this post!

Benki zilizofanikisha ufisadi NYS kuona cha moto

Jeshi la Uganda lazidi kuhangaisha Wakenya Ziwa Victoria

adminleo