Kiongozi wa mashtaka ajikanganya katika kesi ya bangi
Na Richard Munguti
Kiongozi wa mashtaka Abel Amareba amejipata taabani kuhusu shtaka la mihadarati dhidi ya washukiwa watatu.
“Niko na shida na shtaka dhidi ya Baraza Twaha. Ameshtakiwa aje shtaka la kusafirisha misokoto ya bangi pasi kushtakiwa kwa kupatikana akiwa akiwa na bhangi?” akamuuliza hakimu Martha Nanzushi.
Hakinu huyo alimtaka Amareba afutilie mbali shtaka hilo lakini akafafanua kifungu alichoshtakiwa
Twaha alikanusha shtaka la kusafirisha bangi kinyume cha sheria katika mtaa wa Ngara kaunti ya Nairobi.
Hakimu alifahamishwa Twaha alitekeleza kosa hilo baada ya kuachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Makadara.
Ibrahim na Samuel walikabiliwa na mashtaka ya kupatikana na visu mahali pa umma.
Kila mmoja alishtakiwa kwamba walikuwa wanajiandaa kutekeleza uhalifu mtaani Ngara.