Kipusa aliyeuza bima kwa magaidi wa DusitD2 kizimbani
NA RICHARD MUNGUTI
AJENTI aliyeuza bima ya gari lililotumiwa na magaidi kwenye shambulizi katika hoteli ya DusitD2 wiki iliyopita, Alhamisi alifikishwa kortini na kuzuiliwa kwa siku 15.
Kutiwa nguvuni kwa Ziporah Wambui Karanja kumefikisha idadi ya washukiwa waliokamatwa na kuhusishwa na shambulizi hilo hadi 17.
Bi Ziporah Wambui Karanja, ambaye ni ajenti ya kampuni ya Direct Insurance Company Limited, aliagizwa na hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku azuiliwe kwa siku 15 kuwasaidia polisi katika uchunguzi.
Akipinga kuzuiliwa kwa muda huo wote, Bi Karanja alikana kuhusika kwa njia yoyote na uhalifu huo uliopelekea watu 21 kuuawa.
“Mimi ni ajenti wa kampuni ya bima. Nilitekeleza tu kazi yangu ya kuuza bima na sikujua kamwe mteja niliyeuzia bima ni gaidi,” akajitetea.
Mbali na Bi Karanja mshukiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani kuhusiana na shambulizi hilo ni wakili Hassan Abdi Nur anayedaiwa alipokea zaidi ya Sh2 bilioni kupitia benki ya DTB tawi la Eastleigh.
Wengine ni Ismael Sadiq Abitham, Ali Khamisi Ali, Abdinoor Maalima Osmail, Abdullahi Muhumed Hassan na Bi Sophia Njoki Mbogo.
Bi Mbogo ambaye ni Meneja wa DTB tawi la Eastleigh alieleza mahakama ametumikia benki hiyo kwa muda wa miaka minane.
“ Niliajiriwa na benki hii ya DTB miaka minane iliyopita na kwa muda wa miaka minne nimekuwa meneja katika tawi hilo,” alisema Bi Mbogo.
Bi Mbogo alisema Bw Nur pia anahudumu duka la Mpesa na yuko na akaunti katika benki hiyo ya kufanya biashara hiyo.”
Mshukiwa huyo ambaye wakati mwingi alikuwa Analia kortini alieleza mahakama kuwa benki za humu nchini ziliweka mkataba na benki zote kuwa maajenti wake wakuu katika biashara ya Mpesa.
Alisema kuwa mkataba baina ya benki na wateja wa maduka ya Mpesa ni kwa wanaweza kupokea viwango vikubwa vya pesa.
Mahakama ilielezwa na afisa anayechunguza kesi hiyo Bi Monicah Githaiga kwamba polisi wanachunguza mamilioni ya pesa alizokuwa akipokea Bw Nur.
aliomba mahakama imwachilie kwa dhamana akisema – were yesterday arraigned before Senior Principal Magistrate Martha Mutuku.
Mahakama ilielezwa kuwa Bw Nur yuko na maduka ya mpesa na Oktoba mwaka jana aliandikisha akaunti 52 na 47 aliandikisha miezi mitatu ya mwisho yam waka 2018.
Akaunti hizo aliandikisha akitumia simu mbili za rununu na kwamba alipokeas viwango vikubwa vya pesa kutoka Afrika kusini
Mahakama ilielezwa mshukiwa huyu alikuwa anatoa viwango vikubwa vya pesa katika benki ya DTB.
Pesa hizi zilikuwa zinapelekwa nchini Somalia.
Korti ilijuzwa kwamvba pesa hizi zilikuwa zinatumwa baada ya mawasiliano ya simu iliyopigwa mara nyingi.
Abitham, mshukiwa wa pili alikuwa akiwasiliana mara nyingi na gaidi aliyeuawqa Ali Salim Gichunge na mkewe aliye mafichoni Violent Kemunto Omwoyo.