• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Kiwanda cha uchakataji wa samaki kuzinduliwa Kisumu

Kiwanda cha uchakataji wa samaki kuzinduliwa Kisumu

BRENDA AWUOR na ELIZABETH OJINA

WAFUGAJI 5,000 wa samaki kutoka sehemu za Magharibi wanaenda kunufaika kutokana na uzinduliwa wa kiwanda cha uchakataji wa samaki eneo la Kisumu unaotarajiwa mwaka huu wa 2020.

Kiwanda hicho ambacho kitazinduliwa na Rio Fish Limited kitalenga kunufaisha wafugaji wa samaki kutoka maeneo ya Kisumu, Siaya,Homa |Bay, Vihiga, na Kakamega.

Afisa mkuu wa Rio Fish Limited, Bw Dave Oketch, amesema kiwanda hicho kitanufaisha wakulima kutoka vijijini, lengo lao kuu likiwa ni kupata samaki wa kienyeji.

‘’Kiwanda hiki kitafaa wafugaji wote kutoka vijijini kwa lengo la kupata samaki kutoka vijijini,’’ akasema Bw Oketch.

Afisa huyo mkuu ameeleza kuwa chanzo kuu cha kuanzisha kiwanda cha samaki eneo la Kisumu ni kutokana na kuongezeka kwa hamu ya samaki wa kienyeji pamoja na kustawisha ufugaji wa samaki vijijini.

Kiwanda hicho kikiwa kimetengewa kipande cha ardhi chenye ukubwa wa ekari 0.8 eneo la Buoye, Kisumu, kwa sasa kina ofisi pamoja na baadhi ya mashine zitakazotumika katika mchakato wa samaki.

Bw Oketch, ameongeza kusema kuwa kiwanda hicho litaanza kazi Juni 2020.

You can share this post!

Maafisa wanne wakamatwa kwa kuvamia makazi ya Midiwo

Baadhi ya madereva wadai hafla ya kitaifa imewaondolea...

adminleo