• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Korti yadinda kusitisha uchaguzi wa wauzaji wa dawa

Korti yadinda kusitisha uchaguzi wa wauzaji wa dawa

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu Jumatatu ilikataa kusitisha uchaguzi wa wanachama wa chama wenye maduka ya kuuza dawa (KPA) utakaofanyika Alhamisi wiki hii Mombasa.

Akiruhusu uchaguzi huo kuendelea , Jaji Weldon Korir alisema mlalamishi Bw Elias Ndung’u alikaidi agizo la mahakama la Julai 11 kwamba akabidhi KPA nakala za ushahidi lakini akakaidi.

Jaji Korir alisema badala ya Bw Ndung’u kuipa KPA nakala za kesi hiyo aliipeana kwa Bodi inayosimamia wenye maduka ya kuuza dawa.

“Bodi ya KPA ni tofauti kabisa na chama chenyewe,” alisema Jaji Korir.

Wakili wa Elias Ndung’u. Picha/ Richard Munguti

Bw Ndung’u alikuwa ameomba uchaguzi huo usitishwe akidai wanachama zaidi ya 7,000 wa KPA watavurugika kusafiri hadi Mombasa kutoka kila pembe ya nchi hii.

Lakini wakili Wangai Wanjohi anayekitetea KPA alimweleza Jaji Korir kuwa, alikabidhiwa arifa ya kufika kortini Ijumaa saa 11 alasiri na “hakujiandaa itakiwavyo.”

Aliomba korti isisitishe uchaguzi wa Alhamisi kwa “ vile ulipangwa Julai mwaka uliopita na Bw Ndung’u alikuwako. Mbona imemchukua mwaka mmoja kuwasilisha kesi.”

Jaji Weldon Korir. Picha/ Richard Munguti

Bw Wanjohi alisema mlalamishi anataka tu kukisumbua chama na kuomba korti itupilie mbali kesi hiyo.

“ Ni bayana mlalamishi hakutii maagizo ya hii mahakama akikabidhi KPA agizo Julai 11,2019 lakini akakifikia Ijumaa,” alisema Jaji Korir.

Mahakama iliruhusu uchaguzi uendelee na kusema, “ikiwa mlalamishi hataridhika basi kesi hii itasikizwa Oktoba 1, 2019.Mahakama iko na mamlaka na uwezo wa kuharamisha matokeo ya uchaguzi.”

You can share this post!

Jericho Allstars waangushwa na Meltah Kabiria

Lionesses na Simbas zapanda viwango vya raga

adminleo