• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Lazima samaki wote katika ziwa la ufisadi wavuliwe kabla ya 2022 – Uhuru

Lazima samaki wote katika ziwa la ufisadi wavuliwe kabla ya 2022 – Uhuru

Na PETER MBURU

RAIS Kenyatta kwa mara ya kwanza amefunguka  kuwa analenga kukumbukwa kutokana na vita dhidi ya ufisadi atakapoondoka ofisini 2022.

“Ni kitu ambacho nimejitolea kufanya, ni hicho ninachotaka kukumbukwa nacho-vita dhidi ya ufisadi na uwazi na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumiwa namna inavyostahili,” akasema katika mahojiano hayo na BBC.

Alieleza kuwa ukaguzi wa maafisa wa umma utaendelea, akisema hata yeye atakaguliwa.

Aliziomba mahakama kujitolea kusikiza kesi za ufisadi na kuharakisha mchakato, huku akiahidi taifa kuwa watu Zaidi watakamatwa na kushtakiwa.

“Kama serikali na kama mtu binafsi, nimejitolea kwa hivi vita. Huyu ni mnyama, ufisadi ni mnyama ambaye lazima tumuangamize. Kilichosalia sasa ni kwa idara ya mahakama kufanya kazi yake tu na kutoa haki kwa wakenya,” Rais Kenyatta akasema.

“Haijalishi wewe ni nani hata ikiwa wewe ni mmoja wa familia yangu, nimesema kuwa mashirika yako huru kufanya kazi yao,” akaongeza.

Katika mahojiano hayo na BBC, Rais Kenyatta kwa mara ya kwanza alieleza kuwa anataka kukumbukwa kutokana na vita dhidi ya ufisadi atakapoondoka ofisini 2022.

“Ni kitu ambacho nimejitolea kufanya, ni hicho ninachotaka kukumbukwa nacho-vita dhidi ya ufisadi na uwazi na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumiwa namna inavyostahili,” akasema.

Alieleza kuwa ukaguzi wa maafisa wa umma (Lifestyle audit) utaendelea, akisema hata yeye atakaguliwa.

Aliziomba mahakama kujitolea kusikiza kesi za ufisadi na kuharakisha mchakato, huku akiahidi taifa kuwa watu Zaidi watakamatwa na kushtakiwa.

“Kama serikali na kama mtu binafsi, nimejitolea kwa hivi vita. Huyu ni mnyama, ufisadi ni mnyama ambaye lazima tumuangamize. Kilichosalia sasa ni kwa idara ya mahakama kufanya kazi yake tu na kutoa haki kwa wakenya,” Rais Kenyatta akasema.

“Haijalishi wewe ni nani hata ikiwa wewe ni mmoja wa familia yangu, nimesema kuwa mashirika yako huru kufanya kazi yao,” akaongeza.

You can share this post!

Polisi asukumwa jela kwa kumpiga risasi na kumuua mvulana...

Serikali yaahidi kukamata wafisadi zaidi

adminleo