• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:54 PM
Madaktari waonya dhidi ya dawa za kupunguza maumivu ya uke

Madaktari waonya dhidi ya dawa za kupunguza maumivu ya uke

Na MISHI GONGO

MADAKTARI wameonya wanawake dhidi ya kutumia dawa za kienyeji za kupunguza maumivu ya uzazi, wakisema zinachangia vifo vya wajawazito katika maeneo ya Pwani.

Mwenyekiti wa chama cha wakunga na masuala ya kina mama, Dkt Ramadhan Marjan, alisema wanawake wengi hutumia dawa za kienyeji zinazojulikana kama ‘Mihaso’ kusaidia wajifungue upesi, lakini wanakuwa katika hatari ya kuvuja damu nyingi na hata kufariki.

Alieleza kuwa wanawake wengi wanaojifungua kwa mara ya kwanza huchukua hatua hiyo kwa kuogopa kupata maumivu ya uzazi kwa muda mrefu.

Alisema wengi wanayotumia madawa hayo ni baadhi ya wanawake kutoka Kaunti ya Mombasa na ile ya Kwale.

“Wanawake hutofautiana kwa masuala ya uzazi.Kuna wanaochukua muda mrefu kabla njia ya uzazi kufunguka na kuna wale wanaopata maumivu kwa muda mfupi. Ili kuepuka uchungu wengi hutumia njia zinazohatarisha maisha yao,”alisema.

Daktari huyo alisema baadhi za changamoto zinazomfanya mwanamke kupata maumivu kwa muda mrefu ni ikiwa mtoto ni mkubwa na hivyo kuzuia njia ya uzazi kufunguka kwa urahisi.

“Iwapo mtoto ni mkubwa kupita kiasi inalazimu madaktari kuongeza njia wakati wa kuzalisha au hata kumfanyia mama upasuaji.”

You can share this post!

Hofu wafugaji ngamia wakivamia vijiji Kwale

Mifuko ya plastiki inavoingizwa nchini kisiri

adminleo