• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Mahakama yamwachilia Saburi

Mahakama yamwachilia Saburi

Na PHILIP MUYANGA

NAIBU Gavana wa Kilifi, Bw Gideon Saburi ameachiliwa huru kwa dhamana ya Sh200,000 pesa taslimu au dhamana ya Sh500,000 sawa na mdhamini wa kiasi kama hicho.

Hakimu mwandamizi wa Mombasa Elvis Michieka, jana alimwachilia Bw Saburi akisema hakukuwa na sababu mwafaka zilizotolewa na upande wa mashtaka za kutomwachilia mshtakiwa kwa dhamana.

Mahakama pia iliamuru Bw Saburi kuweka paspoti yake mahakamani na kutowasiliana na shahidi yeyote katika kesi hiyo moja kwa moja au kupitia mawakala.

Bw Michieka pia alimwamuru mshtakiwa kufuata maagizo ya serikali ya kukaa mbali na watu, kafyu na maswala yahusianayo na kutembea la sivyo mahakama itakuwa na uhuru wa kufutilia mbali dhamana aliyopewa.

Naibu Gavana huyo wa Kilifi, anakabiliwa na shtaka la kujiweka hadharani akiwa anaugua Covid 19 bila kuchukua tahadhari zifaazo kulingana na sheria ya afya ya umma.

You can share this post!

Wakenya wazidi kuhatarisha maisha yao

NGURE: Kuundwa Baraza la Kiswahili itakuwa tuzo kwa Walibora

adminleo