• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 3:31 PM
Mashirika ya kutetea ushoga hatarini kufungwa

Mashirika ya kutetea ushoga hatarini kufungwa

Na DAVID MWERE

MASHIRIKA ya kigeni yanayotetea ushoga nchini yamo hatarini kupigwa marufuku, baada ya wabunge kuanzisha uchunguzi kuhusu kile wanachokitaja kuwa shughuli zisizo za maadili na zinazokiuka katiba.

Uchunguzi huo ambao unafanywa na Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu Haki na Masuala ya Kisheria (JLAC) ulianzishwa baada ya mbunge maalum Jennifer Shamallah kuandikia bunge.

Kamati hiyo inatarajiwa kutoa mapendekezo baada ya uchunguzi, kuwa baadhi ya sheria zirekebishwe ili kuharamisha ndoa za jinsia moja nchini.

Aidha, uchunguzi unalenga mashirika ambayo yamejitokeza wazi kuwaunga mkono mashoga na wasagaji, hali ambayo Bi Shamallah alisema inahatarisha familia nchini.

Spika wa Bunge la Taifa Justin Muturi aliamrisha kamati hiyo kuchunguza ufadhili wa mashirika hayo na shughuli ambazo yanafanya nchini, kwa lengo la kupendekeza kuwa yafungwe na serikali yakiatikana kuwa na hatia.

Kulingana na Bi Shamalla, ndoa za jinsia moja katika mataifa ambapo mashirika husik yanatoka zimepigwa marufuku kisheria, lakini yanakuja kusukuma ajenda hiyo nchini.

“Mapendekezo yatolewe kuhakikisha kuwa utamaduni wa nchi na imani zetu haziharibiwi na mtaifa ya kigeni. Inashangaza kuwa mashirika hayo yanaleta pesa kuunga mkono ndoa za jinsia moja, wakati mataifa yanapotoka zimekataliwa,” Bi Shamallah akasema.

Kulingana na katiba ya Kenya, kila mtu mzima ana haki ya kuoa mtu bora awe ni wa jinsia tofauti na wote wawe wamekubaliana kufunga ndoa.

You can share this post!

Madiwani Kiambu wafuata ulafi wa wabunge

Kinaya Sportpesa kutuzwa na serikali kisha kuzimwa

adminleo