• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:00 PM
Mchunguzi wa Uswizi atoboa siri ya Anglo-Leasing

Mchunguzi wa Uswizi atoboa siri ya Anglo-Leasing

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Uswizi Dkt Mark Henzline (pichani) aliyeombwa na Serikali achunguze kashfa ya Sh3.8 biloni ya Anglo- leasingeleza alisumulia jinsi aligudua pesa zimefichwa kwenye benki na makampuni yaliyohusika na sakata hiyo.

Dkt Henzline aliikabidhi mahakama inayosikiza kesi dhidi ya wakurugenzi wa makampuni ya Anglo-Leasing ushahidi aliopata.

Dkt Henzline alimweleza hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku kwamba miongoni mwa wakurugenzi aliopata katika uchunguzi wake wameekeza pesa nchini Uswiss ni Mabw Deepak , Rasmi Deepak na Chamanlal Kamani wanaokabiliwa na shtaka la kufanya njama za kuilaghai Serikali Euros 40milioni sawa na Sh3.8bilioni.

Shahidi huyo aliambia korti aliteuliwa na Serikali ya Kenya  kupitia kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu Bw Amos Wako kuchunguza kampuni zilizohusika na kashfa hiyo.

Kampuni ya Anglo-Leasing ilikuwa imepewa kandarasi ya kununulia idara ya polisi mitambo ya kisasa ya mawasiliano na mitambo ya kutengeneza pasipoti kwa lengo la kupambana na ugaidi.

“Afisi ya upelelezi nchini Uswisi ilipokea ombi kutoka kwa Serikali ya kenya ichunguze makampuni ambayo yalikuwa yamehusika na uporaji wa pesa za umma,” Dkt Heinzline alisema.

Alisema baada ya kupokea ombi hilo aliandikia benki kadhaa zilizokuwa zimetumiwa na washtakiwa kuweka pesa walizokuwa wamepokea kwa njia ya undanganyifu kutoka kwa Serikali ya Kenya

Alisema katika barua aliyopewa washtakiwa waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa waziri wa hazina kuu ya kitaifa David Mwiraria, aliyefariki akiwa hospitalini mwaka uliopita.

Hakimu alifahamishwa kuwa ushahidi wote uliopatikana ulikabidhiwa Bw Wako , ambaye sasa ni Seneta wa Siaya.

“Bw Wako  alinipa barua iliyoniteua kuchunguza kashfa hii kwa niaba ya  Serikali ya Kenya,” alisema Dkt Henzline ambaye ni mshirika mkuu katika kampuni ya mawakilkili ya  Laviv ya Uswizi.

“Baada ya kumkabidhi Bw Wako ushahidi huo aliukabidhi afisa mkuu wa tume ya kupambana na ufisadi nchini (EACC) Bw Michael Mubea aliyeanza uchunguzi mara moja,” alisema Dkt Henzline.

Dkt Henzline alisema hayo jana alipotoa ushahidi katika kesi ambapo Mabw Onyonka , Mwangi , Deepak , Rasmi na Chamanlal Kamani wameshtakiwa kwa kuilaghai serikali mabilioni ya pesa katika kashfa hiyo ya Anglo-Leasing.

Shahidi mwingine Mkurugenzi wa shirika la kurejesha mali ya umma iliyoibiwa Bi Muthoni Kimani aliambia mahakama kuwa alimpelekea Dkt Henzline barua ya kumteua kuchunguza kashfa hiyo.

Bi Kimani alisema ilikuwa sherehe kubwa katika afisi ya mwanasheria mkuu baada ya Dkt Henzline kumkabidhi Bw Wako ushahidi aliopata kuhusu kashfa hiyo.

Dkt Henzline alimkabidhi Bw Wako ushahidi naye akamkabidhi afisa mkuu wa tume ya kupambana na ufisadi EACC Bw Michael Mubea uchunguzi zaidi ufanywe,” alisema Bi Muthoni.

Bi Kimani alisema kuwa aliamriwa na aliyekuwa mwanasheria mkuu Profesa Githu Muigai atafute barua za siri zilizokuwa zimeandikiwa kampuni ya Anglo-Leasing na washtakiwa lakini “hakuzipata.”

You can share this post!

Mlima wa nakala za ushahidi kwenye kesi ya wizi NYS

Sukari ya magendo sasa yanaswa Lamu

adminleo