• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Moi ni babangu kisiasa – Ruto

Moi ni babangu kisiasa – Ruto

“Tunampa mkono wa buriani kiongozi mashuhuri wa nchi yetu na baba yetu. Nasema baba yetu nikiwakilisha mamia ya maelfu ya watu ambao japo hawakuwa wanawe wa damu, ni watoto wa kiongozi huyu mkubwa,” akasema Naibu Rais Dkt Willima Ruto.

“Tunashukuru familia ya Mzee Moi kwa kutukubalia Moi kuwa baba yetu. Mmekuwa wakarimu kwa kuwa tulikuwa na wazazi wetu lakini bado tulikuwa watoto wa baba yenu. Leo tunamzika mpenda-nchi.

“Kwetu tuliowajua wakati alikuwa karibu kuondoka uongozini, na ambao tulikuwa vitinda mimba wake kisiasa, tulishuhudia na kusoma vitu vingi kutoka kwa Moi. Jinsi imesemwa, kuhusu masuala ya mapenzi yake kwa elimu yalimsukuma kuboresha viwango vya elimu zaidi. Leo hii Kenya inajivunia kuwa na wananchi walioelimika na wanaofanya kazi sehemu tofauti za dunia kutokana na hilo.

“Tunaweza kusema bila shaka yoyote kuwa Moi ndiye aliyeunda kituo chenye adabu sana cha jeshi Kenya, Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla.

“Na mwisho Moi aliunda chama imara cha kisiasa cha Kanu kilichomsaidia kuunganisha nchi na kujumuisha jamii zote, akifanya nchi kutotumbukia katika vita na utengano kama mataifa mengine. Moi alitufunza umoja. Sisi tulifuzu kutoka shule ya kisiasa ya Moi na tunajivunia,” akamalizia Dkt Ruto.

You can share this post!

Wajukuu wasema Moi alitenga muda kuwa nao

Shida kivukoni kufuatia feri 2 kuondolewa

adminleo