• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:55 AM
Motoni kwa kumpiga na kumng’oa meno binamu ya Maraga

Motoni kwa kumpiga na kumng’oa meno binamu ya Maraga

Na JOSEPH NDUNDA

MWANAMUME aliyempiga binamu ya Jaji Mkuu David Maraga na kumng’oa meno matatu wakizozania watoto, Jumanne alipatikana na hatia ya kusababisha jeraha la kudumu.

Zedekiah Omari anaweza kufungwa jela maisha baada ya Mahakama ya Makadara kumpata na hatia ya kumjeruhi shemeji yake Walter Makori.

Hakimu Mkuu Mkazi Eunice Suter alisema mahakama ilithibitishiwa kwamba Omari alitenda kosa hilo Novemba 22, 2014 nje ya nyumba yake mtaani Utawala, Nairobi.

Omari pia alikuwa ameshtakiwa kwa kuharibu gari la Makori lakini mahakama ikamwondolea shtaka hilo ikisema hakukuwa na ushahidi.

Mahakama ilifahamishwa kwamba Makori na ndugu yake Isaac Bosire walikuwa wameenda kwa Omari kumuokoa dada yao Hellen Kwamboka aliyewaita akidai mumewe alikuwa akimpiga pamoja na watoto wao.

Watoto na mama yao walikimbia na kuingia ndani ya gari lakini Omari alitoka ndani ya nyumba akipiga kelele na kuwaita mashemeji wezi.

Baadaye Omari alianza kupura gari kwa mawe na kumgonga Makori kwenye taya akapoteza fahamu kwa muda.

You can share this post!

Vyama viwe vikimchagua Rais, wabunge wapendekeza

Dongo Kundu: Serikali yatoa Sh100m kulipa walioathiriwa

adminleo