Wauzaji wa unga wameonywa dhidi ya kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwa kusingizia ushuru wa asilimia 16 unaotozwa mafuta.
Akiongea na wanahabari Jumanne, Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri alidai kuwa ushuru huo hauna athari kwa watengenezaji wa unga, hivyo, hawafai kuongeza bei ya unga.
Hata hivyo, chama cha wasagaji wa unga(CMA) tayari kimeonya kuwa kitaongeza bei ya unga kwa sababu ya ongezeko la bei ya mafuta.
Bei ya juu ya mafuta inaathiri gharama ya usafirishaji sio tu wa mahindi, lakini pia unga uliosagwa.
Waziri huyo alisema kiwango cha mahindi yaliyovunwa nchini kimo juu ikilinganishwa na msimu uliopita, hivyo hakuna upungufu wa mahindi.
Alisema msimu huu magunia milioni 46 yatavunwa ikilinganishwa na magunia milioni 40 yaliyovunwa msimu