Habari Mseto

Mwanamke alazwa akiwa na majeraha ya moto, familia 18 zaachwa bila makao

June 25th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na SAMMY KIMATU

[email protected]

MWANAMKE amelazwa katika Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) baada ya kuchomeka huku watoto wawili wakiokolewa wakati moto mkubwa ulitokea usiku wa kuamkia Jumanne na kuwacha familia 18 bila makao.

Mali ya thamani ya pesa isiyojulikana iliteketea na kubakia kuwa majivu.

Kisa hicho kilitokea katika eneo la Crescent Cluster A mtaani wa mabanda wa Mukuru-Kaiyaba ulioko kwenye tarafa ya South B kwenye eneo bunge la Starehe, Kaunti ya Nairobi.

Pokisi wallimtambua mwanamke huyo kwa jina Bi Mary Achieng Mbinga mwenye umri wa miaka 49 anayeuza sambusa mtaani humo na hujulikana kwa jina mama Clinton.

“Anauguza majeraha kichwani, mikononi na miguuni lakini watoto waliokolewa wqakiwa salama, ” akasema mwenyekiti wa mtaa huo Bw Jacob Ibrahim.

Kwa muhibu wa mwathiriwa, Bi Esther Gitau almaarufu Mama Chege ambaye ni afisa wa masuala ya watoto wa kujitolea, moto ulianza katika nyumba moja kabla ya kuenea kwa kasi ukichochewa na upepo.

Hakuna kilichookolewa

Bi Chege alisema hakuokoa chochote kulingana na kasi moto huo ulivyosambaa pamoja na moshi.

Bw Ibrahim alidai moto ulisababishwa na hitilafu ya stima baada ya waya kubeba nguvu kupita kiasi.

Magari mawili ya zimamoto na ambulensi ya serikali ya Kaunti iliwasili upesi na kuudhibiti moto huo.