• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Mwanamke wa ‘simu ya kifo’ kutafutiwa wakili na serikali

Mwanamke wa ‘simu ya kifo’ kutafutiwa wakili na serikali

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE anayedaiwa alimuua mumewe kwa sababu ya kuongea na ‘mpenzi wa pembeni’ kwa simu saa tano usiku amefikishwa mbele ya Jaji James Wakiaga.

Hata hivyo, Zaitun Abdul hajasomewa shtaka kwa sababu hakuwa na wakili wa kumtetea.

“Hii ndiyo mara ya kwanza ya mshtakiwa kufikishwa kortini. Hana wakili wa kumtetea na hivyo basi hahitajiki kujibu shtaka dhidi yake,” kiongozi wa mashtaka Bi Wangui Gichuhi amemweleza Jaji Wakiaga.

Bi Gichuhi ameomba mshtakiwa ajulishwe shtaka dhidi yake kisha apelekwe katika gereza la Wanawake la Langata jijini Nairobi.

Jaji Wakiaga amemweleza mshtakiwa “shtaka linalokukabili wahitaji wakili kwa vile ukipatikana na hatia utanyongwa ama kusukumwa jela maisha. Serikali itakutafutia wakili na utarudishwa kortini Mei 11, 2020.”

Jaji Wakiaga ameamuru mshtakiwa apelekwe gereza la wanawake la Langata atakapozuiliwa hadi wiki ijayo.

Zaitun inadaiwa alitofautiana na mumewe usiku wa Aprili 17, 2020, baada ya mhanga kupokea simu kutoka kwa mwanamke mwingine.

Baada ya kuzugumza mambo ya mahaba na mpiga simu, Zaitun alianza vurugu lakini hiyo ndiyo ilikuwa siku yao ya kurushiana cheche za maneno.

Mahakana ya Milimani awali ilifahamishwa usiku huo wa Aprili 17 uliokuwa umeanza taratibu baina ya wanandoa uligeuka kuwa wa majonzi Zaitun alipoangamiza uhai wa mumewe.

“Wawili hao walikuwa wanazozana mara kwa mara huku kila mmoja akidai mwenzake sio nwaminifu,” Mahakama ilifahamishwa.

Kisa hicho kilichotokea katika mtaa wa mabanda wa Lindi, Kibra katika Kaunti ya Nairobi kiliwaacha wengi na mshangao.

Hakimu mkazi Carolyne Muthoni Nzibe alifahamishwa na viongozi wa mashtaka Winnie Moraa na Angela Fuchaka kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma hajaamua shtaka atakalomfungulia Zaitun.

You can share this post!

COVID-19: Visa vipya leo ni 25 idadi jumla nchini ikifika...

Mkurugenzi wa Skyways, wazazi wawatunuka walimu chakula na...

adminleo