Mwanasiasa ataka serikali isambazie wakulima mbolea
MWENYEKITI wa Jubilee Kaunti ya Kirinyaga, Mureithi Kang’ara, ameitaka serikali kusambaza mbolea ya gharama nafuu kwa wakulima ili itumike msimu huu wa upanzi.
Bw Kang’ara alisema mvua ambayo sasa inashuhudiwa itawanufaisha wakulima kipindi hiki cha upanzi na serikali haifai kuchelea kutoa mbolea hiyo.
Alikuwa akiongea Jumatatu, Machi 31, 2025 mjini Makutano ambapo alimwaambia Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ahakikishe kuwa kusambazwa kwa mbolea hiyo kunafanyika haraka.
Aliongeza kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kuna usalama wa chakula nchini iwapo wakulima watapigwa jeki na kusambaziwa mbolea kwa wakati tena mbolea bora.