Niachilie nikawapikie watoto, mama amlilia hakimu katika shtaka la wizi
Na RICHARD MUNGUTI
MWANAMKE aliiyeshtakiwa Jumatatu kwa kufanya njama za kuibia benki ya Jamii Bora Sh3,088,000 Jumatatu aliomba aachiliwe kwa dhamana “akapikie watoto.”
Mary Polyne Khagali na Aquinata Imbwaka walifikishwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi na kusomewa mashtaka manne.
Shtaka la kwanza lilikuwa la kufanya njama za kuibia benki hiyo Sh3,088,000. Aquinata alikana aliiba Sh600,000 .
Alikabiliwa na shtaka lingine la kuweka katika akaunti yake Sh840,000 akijua zimeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.
Naye Mary Khagali alikana alikutwa ameweka katika akaunti yake Sh740,000 akijua zimeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.
“Naomba uniachilie kwa dhamana nikawapikie watoto wangu, mheshimiwa. Tangu niwekwe korokoroni sijui hata yule mchanga anakula nini. Waonee wanangu huruma na uniachilie kwa dhamana,” alirai Aquinata.
Andayi aliwaachilia kwa dhamana ya Sh200,000 pesa tasilimu kila mmoja.
Kesi itasikizwa Aprili 23.