Nyumba 100 zateketea Mukuru
NA SAMMY KIMATU
NAIROBI
ZAIDI ya watu 300 katika mtaa mmoja wa mabanda kaunti ya Nairobi walikesha nje penye baridi kali baada ya nyumba zaidi ya nyumba100 kuteketea.
Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Mukuru-Hazina katika kaunti ndogo ya Starehe.
Naibu wa Chifu wa eneo hilo, Bw Nelson Kambale aliliambia taifa kuwa moto huo ulianzia katika nyumba, ambayo mwanamke alikuwa akipika na alikuwa ametoka kununua mboga.
Mbali na nyumba, vibanda vya biashara viliteketea pia. Mhasiriwa,
Mwathiriwa, Bi Charity Kawira, 45 alisema nyumba yake ilijaa moshi na hangeweza kuokoa chochote kwani alikuwa ameenda kununua bidhaa za kuuza katika kibanda chake.
Isitoshe,magari matatu ya kuzima moto kutoka kaunti ya Nairobi yalifika haraka kupambana kuuzima moto huo.
Walakini, malori mawili kutoka kwa huduma ya jiji ya Nairobi (NMS) ilileta maji na kusaidia kuyaongeza maji
.”Vijana walisaidiwa sana kwa kubomoa nyumba zingine kuzuia moto usienee zaidi.
Kadhalika, waporaji katika eneo la tukio walinyunyizia maji maafisa wa polisi ambao walikuwa katika eneo la tukio.
Chifu Kambale ameongeza kuwa mtu mmoja alijeruhiwa wakati wa tukio hilo.
Kadhalika, wahasiriwa wanaomba msaada.