Polisi ashtakiwa kuiba vita vya Sh6 milioni
Na Richard Munguti
Afisa wa polisi alishtakiwa kwa uvunjaji wa ghala na kuiba viatu vinavyovaliwa na maafisa wa utumishi kwa wote vya thamani ya Sh6.4 milioni.
Konstebo Denice Onyango Okkng’o alikana shtaka la wizi wa viatu 1.826 vya maafisa wa polisi wanaume na viatu 398 vya polisi wa kike.
Jumla ya thamani ya viatu hivyo ni Sh6,454, 342. Okong’o akifikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Kibera Nairobi Bw Abdulkadir Lorot.
Mshtakiwa aliwakikishwa na wakili Harun Ndubi. Bw Ndubi aliomba mshatakiwa aachiliwe kwa dhamana akifichua ameoa wake wawili na wamejaliwa watoto watano.
“Naomba hii mahakama imwachilie mshtakiwa kwa dhamana ya Sh100000.Ameoa wake wawili.Wako na watoto watano na maujukumu yake ni mengi,” Bw Ndubi alimsihi hakimu.
Akaongeza kusema wakili huyo.”Naomba korti imwachilie arudi nyumbani akaendelee na majukumu yake.”
Kiongozi wa mashtaka alipinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana ya Sh100000 akisema ,” kesi hiyo itaunganishwa na nyingine ambapo washukiwa wengine wameachiliwa kwa dhamana ya Sh200000.
Aliomba kesi hiyo itajwe Septemba 1 2020 iunganishwe na hiyo ya hapo awali. Hakimu alimwachilia kwa dhamana ya Sh200000.
“Nimetilia maanani mawasilisho yote ya upande wa mashtaka na utetezi na kufikia uamuzi sharti mshtakiwa apewe dhamana,” Bw Lorot alisema.
Mahakama ilimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya Sh200000 kama ilivyo katika kesi iliyowasilishwa hapo awali.
Bw Lorot alitenga kesi hiyo kutajwa Septemba 1.
Okong’o alidaiwa alitekeleza wizi huo usiku wa Agosti 8-9 2020 katika ghala lililoko eneo la Viwandani Nairobi