Ruto aendea baraka za 2022 kwa wazee
NA MWANDISHI WETU
Naibu Rais Dkt William Ruto aliongoza kundi la viongozi wa Jubilee kutoka Bonde la Ufa katika mkutano uliohusisha wazee wa jamii ya Kalenjn eneo la Kapsisiywa, Kaunti ya Nandi, uliolenga kutafuta barakaza wazee ili awanie kiti cha urais hapo 2022.
Msafara wa Naibu Rais ulifika nyumbani kwa James Bassy, mwanachama wa baraza la wazwee wa Talai na kuzungumza kwa muda wa saa 3, kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa mbili asubuhi.
Wazee wa Talai wa ukoo wa aliyekuwa kiongozi wa jamii ya Nandi miaka ya ukoloni Koitalel arap Samoei, wanaheshimiwa sana na wanaaminika kuwapa baraka na mwongozo watu wakiwepo wanasiasa.
Wakati mahakama kuu ilitupilia mbali uchaguzi wa mwaka wa 2017 Rais Uhuru Kenyatta na Naibu William Ruto walitembelea milima ya Nandi ambapo wazee wa Talai walifanya ibada ya kitamaduni kuwabariki.
Naibu katibu wa chama cha Jubilee Caleb Kositany alisema kwamba kulikuwa na mkutano lakini hakutaja ulikuwa unahusu nini.
“Naibu Rais aliweka mkutano na wazee wa Talai lakini yalikuwa ni mambo ya kibinafsi,” alisema Bw Kositany.