• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Sakaja kuongoza kamati ya seneti kuhusu janga la corona

Sakaja kuongoza kamati ya seneti kuhusu janga la corona

 

Na CHARLES WASONGA

SENETA wa Nairobi Johnson Sakaja ameteuliwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya seneti itakayofuatilia utendakazi wa Kamati ya Kitaifa ya Dharura (NERC) inayoshughulikia janga la Covid-19.

Naye Seneta Maalum Sylvia Kasanga aliteuliwa naibu mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wanachama saba iliyoundwa kufuatia hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa wengi Kipchumba Murkomen.

Wawili hao waliteuliwa kwenye mkutano wa kamati hiyo iliyofanyika Jumatano kwa njia ya video, kutii kanuni ya watu kutokaribiana ili kudhibiti kueneo kwa virusi vya corona.

“Kamati hiyo itafuatilia hatua ambazo zimechukuliwa na serikali ya kitaifa na zile za kaunti kwa lengo la kudhibiti kuenea na athari za virusi vya corona kote nchini,” Bw Murkomen, ambaye ni seneta wa Elgeyo Marakwet alisema.

Wanachama wengine wa kamati hiyo ni pamoja na; Seneta wa Trans Nzoia Michael Mbito, Mithika Linturi (Meru), Okong’o Omogeni (Nyamira), Mohammed Faki (Mombasa), na Seneta Maalum Abishiro Halakhe.

Maseneta wote 28 waliokuwemo kikaoni waliunga mkono kubuniwa kwa kamati hiyo na kuitaka kupendakeza sera na sheria ambazo zitawalinda Wakenya kutokana na makali ya ugonjwa huo hatari. Waliwataka wenzao wa Bunge la Kitaifa pia kuunda kamati kama hiyo.

You can share this post!

Binti apiga hatua katika biashara ya bima licha ya...

Waliomkejeli Brenda wakamatwe – Kagwe

adminleo