• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 7:55 PM
Serikali yataka maoni ya Wakenya kuhusu Sheria ya Data

Serikali yataka maoni ya Wakenya kuhusu Sheria ya Data

Na FAUSTINE NGILA

SERIKALI kupitia Wizara ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano imewaomba Wakenya wajitokeze kuchangia kuhusu kubuniwa kwa kanuni mpya za kulinda data.

Katika ujumbe uliotumwa kwa vyombo vya habari jana, wizara hiyo ilieleza kuwa kanuni hizo zitawiana na Sheria ya Kulinda Data ya 2019, ambayo imetoa mwongozo kuhusu jinsi data ya mifumo ya kusajili wananchi inafaa kusimamiwa.

Data hiyo imehifadhiwa katika mfumo wa Huduma Namba, ambao unalenga kunasa taarifa za Wakenya, kwa dhamira ya mipango ya kifedha ya taifa hili.

“Wizara hii inawaalika Wakenya kuwasilisha maoni yao kuhusu kubuniwa kwa kanuni hizi. Maoni haya yanaweza kuwasilishwa kupitia kwa maandishi au maongezi,” imesema serikali kwenye stakabadhi hiyo.

Watakaowasilisha maoni yao kupitia mjadala wanatakiwa kuhudhuria mjadala wa kitaifa kuhusu suala hilo jijini Nairobi na Mombasa na mjini Nakuru hapo Februari 27, 2020.

“Mkutano wa Nairobi utaandaliwa katika jumba la KICC, Mombasa utafanyika katika majengo ya Kenya School of Government ilhali Nakuru utakuwa katika Old Town Hall,” imeeleza.

Watakaopenda kuandika maoni yao wanaombwa kutuma barua zao kwa Katibu katika wizara hiyo kabla ya Machi 2, 2020. Pia, wanaweza kuzituma kwa washirikishi wa kaunti, manaibu wao au kutuma baruapepe moja kwa moja kwa [email protected].

You can share this post!

Supkem kutoa orodha ya maajenti wa safari za kwenda Hija

Sonko aendelea kuchapa kazi licha ya kufungiwa nje ya ofisi

adminleo