• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 3:13 PM
Uamuzi kuhusu ushoga na usagaji kutolewa Mei

Uamuzi kuhusu ushoga na usagaji kutolewa Mei

Na RICHARD MUNGUTI

UAMUZI wa kuhusu iwapo ndoa za jinsia moja zitaruhusiwa humu nchini uliahirishwa hadi Mei 24.

Walalamishi waliofika katika Mahakama Kuu ya Milimani Nairobi kujua hatma ya kesi yao waliondoka wakiwa wamevunjika mioyo kwa vile walikuwa na matumaini hawatajificha tena bali watafanya mambo yao kwa uwazi.

Jaji Enoch Chacha Mwita aliwaeleza walalamishi waliowasilisha kesi hiyo mahakamani kwamba uamuzi hauko tayari.

“Uamuzi wa kesi hii hauko tayari. Baadhi ya majaji waliosikiza kesi hii wamekuwa wakihusika na kesi nyingine na hawajakamilisha kuandaa uamuzi huu,” alisema Jaji Mwita.

Jaji Mwita aliwaomba msamaha mawakili waliohusika katika kesi hiyo wakiongozwa na wakili mwenye tajriba ya juu Bw Paul Muite.

Walalamishi katika kesi hiyo wanasema chini ya katiba kila mmoja yuko na uhuru kuchagua jinsia atakayofunga ndoa nayo.

Wahusika wanaomba mahakama kuu iamuru mashoga wakubaliwe kufunga ndoa wanaume kwa wanaume .

Pia wasagaji wanaomba wakubaliwe kufunga ndoa baina yao.

Lakini kesi hiyo imepingwa vikali na makundi ya Wakristo wakisema masuala hayo ni kinyume cha mafundisho ya Bibilia Takatifu na pia yanakinzana na utamaduni wa jamii mbalimbali nchini.

Uamuzi huo ulikuwa umehudhuriwa na walalamishi na wanahabari wa kimataifa waliofurika katika Mahakama Kuu ya Milimani wakiwa tayari kupeperusha uamuzi huo.

You can share this post!

BI TAIFA FEBRUARI 23, 2018

BI TAIFA FEBRUARI 24, 2019

adminleo