• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 1:33 PM
Vijana wapendekeza wafundishwe kuhusu ngono na uzazi

Vijana wapendekeza wafundishwe kuhusu ngono na uzazi

Na FARHIYA HUSSEIN

VIJANA eneo la Mombasa, wametaka maswala kuhusiana na masomo ya ngono kuzingatiwa zaidi shuleni.

Vijana hao kati ya umri wa miaka 18-24 wametaka maswala kuhusiana na Maradhi ya Ukimwi, upangaji uzazi na swala la hedhi kuzingatiwa kwa kina shuleni.

Katika Kaunti ya Mombasa, Michael Omondi alisema vijana wengi huwa wanategemea mitandao ya kijamii kwa vile maswala kama haya huzingatiwa shuleni mara moja moja.

“Shuleni maswala haya huzungumziwa wakati wa mashauriano baina ya wanafunzi na walimu, inapaswa kuzungumziwa kwenye madarasa pia ili tujifunze mengi kuhusiana na jambo hii. Kwa mfano, mimi binfsi ningefurahia kujua mengi kuhusiana na maradhi ya Ukimwi,” akasema Omondi.

Alisema kuwa vijana wengi hujipoteza kwa kutumia mitandao wa kijamii kwa lengo la kutaka kujifunza mengi kama maswala ya AASRH ingezingatiwa kwa kina shuleni itawafaidi vijana hawa.”Wengine wanapendelea kujifunza kupitia kwa wazazi wao ingawa wengi wao hujificha kimya kimya na kutozungumzia kile wanachopitia, ni muhimu sana maswala haya kuwekwa wazi shuleni,” akasema Omondi.

Kulingana na ripoti ya mwaka wa 2019, iliotolewa na Jiactivate ilionyesha asilimia 62 walipata mafunzo kuihusiana na ASSRH na mahusiano baina ya mtoto wa kike na kiume kwa waliohudhuria shule za serikali na asilimia 48 wale waliohudhuria shule za kidini walipata mafunzo hayo.

Awino Nancy kutoka Kaunti ya Kilifi, alisema ni muhimu wasichana kupata mafunzo shuleni kuhusu maswala ya hedhi kwa vile wengi wao hupata wakati mgumu kuendelea na masomo.

” Kati ya miaka 13-17, tunaanza kuwa na mabadiliko mwilini na wengi wetu huwa hatupenedelei kuzungumzi haya maswala hadharani. Lakini mafunzo kama haya yakisisitizwa shuleni watoto wa kike watafaidika na kusaidika,” akasema Nancy.

Aliongezea kuwa wengi hawana mafunzo kuhusu jinsi ya kutumia visodo lakini programu ya kuwafunza mambo kama haya yakianzishwa shuleni haswa kwenye makao duni na mashinani watafaidika.

“Matineja wengi hupata mimba wakiwa shuleni, na wengi wao hutegemea mitandao ya kijamii kujieleza maswala kadhaa.Wachache huzungumza na wazazi wao ili kupta ushauri na ingekuwa vyema wakifunzwa shuleni na si kutegemea mitandao ya kijamii,” akasema Nancy.

Aidha, imefahamika kwamba vijana wengi hawazungumzi na kuw wazi n wazazi ikifika ni haya maswala.

“Tumeanzisha programu itakayohusisha mafunzo ya kijinsia eneo la Kilifi. Hii ni kwa sababu kaunti hiyo ina idadi kubwa ya matineja wanaopata mimba shuleni na itakuwa vyema kuwahusisha kwa haya maswala,” alinena Mwenyekiti wa Kundi la Jiactivate, Bw Grayson Marwa.

You can share this post!

‘Referenda yafaa kujali maslahi ya wananchi, si...

Vijana wanalipa mikopo bila matatizo – Ripoti

adminleo