• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 5:23 PM
Wafanyabiashara Uganda wagoma kupinga mfumo mpya unaowalazimu kulipa ushuru wa juu

Wafanyabiashara Uganda wagoma kupinga mfumo mpya unaowalazimu kulipa ushuru wa juu

NA MASHIRIKA

KAMPALA, UGANDA

WAFANYABIASHARA Uganda Jumatano waligoma kupinga utekelezaji wa mfumo mpya ambao utawalazimisha kulipa ushuru wa juu.

Wafanyabiashara wengi wanaamini kuwa mfumo huo mpya utatatiza shughuli zao.

Mfumo wa Kielektroniki wa Kupokea na Kutuma kodi (EFRIS) ulizinduliwa na mamlaka ya ushuru mnamo Januari 2021 ili kufuatilia mauzo na kodi.

Mfumo huo ulitekelezwa hivi majuzi jambo ambalo liliwafanya wafanyabiashara hao kugoma.

Wiki iliyopita, wafanyabiashara mjini Kampala na miji mingine mikuu walifanya maandamano ya siku mbili kupinga utekelezwaji wa mfumo huo.

Haya yanajiri huku Rais wa Uganda Yoweri Museveni akijiandaa kukutana na viongozi wa wafanyabiashara wanaogoma ili kutafuta njia za kusuluhisha malalamishi yao.

Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara Kampala (KACITA Uganda) na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Uganda (FUTA) walisema kwamba wanapanga kuenda kuchukuliwa vipimo vya corona kabla ya kukutana na rais huyo.

Katika ombi kwa Waziri wa Fedha, Matia Kasaija, KACITA ilielezea malalamishi kadhaa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji unaoendelea wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) na kuwaingiza wafanyabiashara kwenye mfumo wake mpya wa kidijitali.

Msemaji wa URA Ibrahim Bbosa hakupokea wala kujibu simu alipotafutwa ili kutoa maoni.

Imebainika kuwa wafanyabiashara katika miji ya mikoani kama vile Fort Portal, Mbarara na Mbale kwa sababu mbalimbali walisusia maandamano hayo.

Akiwa Masaka, Bw Ali Pio Mukasa, mwakilishi wa wafanyabiashara wa Chuo Kikuubo katika Chama cha Wafanyabiashara wa Jiji la Masaka (MACITA), alisema walisusia mgomo huo wiki jana baada ya Bw Ahmed Kateregga, naibu kamishna mkazi wa jiji kuwahakikishia kuwa suala hilo lingetatuliwa.

  • Tags

You can share this post!

Barcelona yalia na kusaga meno huku Dortmund wakipepea Uefa

Nakhumicha ataka hospitali zikubali NHIF akisema madeni...

T L