Wakazi walalamikia ufujaji wa fedha za ujenzi barabara
MAMIA ya wakazi wa eneo la Acacia mjini Kitengela, Kaunti Ndogo ya Kajiado Mashariki, walishiriki maandamano ya Amani Jumatatu, Juni 17, 2024 wakilalamikia wanachotaja kama kazi duni inayofanywa na mwanakandarasi na ufujaji wa fedha za umma.
Wakazi hao waliojawa na ghadhabu huku wakiwa wamebeba mabango ya kumsuta mwanakandarasi husika na diwani wa eneo hilo, walisema licha ya Serikali ya Kaunti ya Kajiado kutengea barabara hiyo mamilioni katika bajeti ya 2023/2024, sehemu kubwa ya barabara hiyo haipitiki na imejaa vumbi.
“Tunataka ujenzi wa barabara hii urudiwe. Mwanakandarasi alishirikiana na uongozi eneo hili katika njama za kufuja mali ya umma,” alisema Karani wa Ujirani wa Acacia, Chris Waithanje.
Bw Joseph Ole Lenku ndiye Gavana wa Kaunti ya Kajiado.
Gavana Lenku anahudumu awamu yake ya pili nay a mwisho.