• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Wakenya wengi wahudhuria kongamano la dunia kuhusu miji Abu Dhabi

Wakenya wengi wahudhuria kongamano la dunia kuhusu miji Abu Dhabi

Na MAGDALENE WANJA

KENYA ni baadhi ya nchi ambazo zimeandikisha idadi kubwa ya watu wanaohudhuria Kongamano la Dunia kuhusu Miji – World Urban Forum – ambalo linafanyika jijini Abu Dhabi, Milki za Falme za Kiarabu (UAE).

Watu 740 kutoka nchini Kenya tayari wanahudhuria kongamano hilo ambalo lilifunguliwa rasmi mnamo Februari 8, 2020.

Kongamano hilo linanuia kuangazia mambo ambayo yanaikumba miji ambayo ni pamoja na kukua kwa idadi ya watu wanaohamia mijini, ujenzi, uchumi na mabadiliko ya tabianchi.

Wanaohudhuria wanaongozwa na katibu katika Wizara ya Makazi na Ustawishaji wa Miji Bw Charles Hinga.

Hili ni kongamano la 10 la World Urban Forum (WUF 10).

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa la UN-Habitat Bi Maimunah Mohd Sharif, mabadiliko mengi yamefanyika tangu kongamano la kwanza mnamo mwaka 2002.

“Uhamasishaji miji umetambulika sasa kama mojawapo ya mitindo mipya ambayo inaleta mabadiliko katika maisha ya kila siku,” akasema Bi Mohd.

Baadhi ya wanaohudhuria ni pamoja na msimamizi wa kituo cha vijana cha Mathare One-Stop Youth Centre Isaac Mutisya Muasa anayejulikana kama ‘Kaka’.

Anatambulika kutokana na juhudi zake za kubadilisha maisha ya vijana kupitia kituo cha uhifadhi wa mazingira cha Mathare Environmental Conservation Youth Group ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 1997.

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Mwalimu Namanda

Tuju apata ajali akiwa safarini kuhudhuria mazishi ya Moi

adminleo