Habari Mseto

Washukiwa 7 kuhusu ajira hewa za ughaibuni wakamatwa

Na TITUS OMINDE  August 28th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

WASHUKIWA saba wanaohusishwa na ongezeko la visa vya ulaghai wakijifanya maajenti wa kazi katika nchi za kigeni mjini Eldoret, wametiwa mbaroni.

Washukiwa hao walikamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na makachero kutoka idara ya Upelelezi wa Jinai na Uhalifu (DCI).

Polisi walinasa washukiwa hao katika afisi zao wakiendeleza shughuli zao za kila siku.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi alisema kuwa kukamatwa kwao kumefuatia vidokezo kutoka kwa wananchi kuhusiana na shughuli za kutiliwa shaka za mashirika husika.

Maafisa wa upelelezi walipovamia afisi hizo walipata watu ambao walikuwa wakitafuta kazi wakiwa wamepanga foleni katika baadhi ya ofisi hizo za maajenti walaghai kwa ahadi ya kuajiriwa ughaibuni.

Kulingana na Bw Mwanthi, mashirika mengi ya kutoa ajira hizo jijini humo yamekuwa yakifanya kazi bila vibali halali.

Bw Mwanthi alifichua kuwa washukiwa zaidi ya kumi walifanikiwa kukwepa mtego wa polisi