• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:12 PM
‘Watu wengi wataanagamia kwa vileo haramu, pombe ikiongezewa ushuru’

‘Watu wengi wataanagamia kwa vileo haramu, pombe ikiongezewa ushuru’

Na BERNARDINE MUTANU

Watengenezaji wa pombe wameonya kuwa kuongezwa kwa ushuru kwa pombe kutazua ongezeko la pombe haramu nchini.

Jumanne, chama cha watenegenezaji wa pombe(ABAK) kilisema ongezeko la bei ya pombe halali litafanya watu kunywa pombe ya bei ya chini.

Hatua hiyo sio tu itaathiri mapato ya watengenezaji halali wa pombe, lakini itaathiri afya ya watumiaji wa pombe na mapato ya serikali.

Waziri wa Fedha Henry Rotich alipendekeza kuongeza ushuru kwa pombe, sigara na mafuta.

Chama hicho ambacho kinashirikisha Kenya Breweries Limited na Heineken East Africa kimetaka Hazina ya Fedha kuambatisha ushuru wake na ushuru unaotozwa na mataifa mengine eneo la Afrika Mashariki kwa bidhaa hiyo.

Pia, kilisema hatua hiyo itaongeza viwango vya pombe ghushi itakayoagizwa nchini, wakati ambapo serikali inakabiliana na bidhaa hizo katika soko la humu nchini.

You can share this post!

Likizo ya lazima kwa wakuu wa NCPB

Msiingize siasa kwa sukari ya sumu, wanasiasa waonywa

adminleo