Habari Mseto

Wazee wanaodaiwa kuwa wachawi wazidi kuuawa Kwale

October 24th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na FADHILI FREDRICK

HOFU imetanda katika Kaunti ya Kwale baada ya visa vya mauaji dhidi ya wazee kwa madai ya kuwa wachawi kuongezeka.

Kulingana na takwimu za idara ya polisi, watu zaidi ya 42 wameuawa kwa njia tatanishi, wengi wao wakiwa wazee wakisingiziwa kuwa wachawi.

Kamshina wa Kaunti, Bw Karuku Ngumo alisema visa hivyo vimetekelezwa na kuripotiwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari mwaka huu.

Visa vinaripotiwa kukithiri mno maeneobunge ya Kinango na Lunga Lunga ambapo jamii nyingi zinazoishi mashambani huhusisha matukio watu kuugua na vifo vya ghafla na uchawi.

”Mizizi ya imani ya uchawi imekita katika jamii na imeathiri maendeleo makubwa na kusababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia. Suluhisho inapaswa kupatikana,” akasema,

 

Alisema madai ya uchawi hayawezi kuupuzuliwa mbali, akidhani sababu kubwa ni migogoro ya ardhi na urithi wa mali umesababisha kushambuliwa kwa kwa visingizio vya uchawi.