• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 4:23 PM
Walionaswa na kamera za CCTV wakitekeleza wizi kimabavu wakamatwa

Walionaswa na kamera za CCTV wakitekeleza wizi kimabavu wakamatwa

Na CHARLES WASONGA

WASHUKIWA wanne ambao wanahusishwa na kisa cha wizi wa kimabavu mchana peupe katika barabara ya Lenana, Nairobi wamekamatwa na maafisa wa upelelezi.

Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) Jumatatu imefichua kuwa washukiwa hao ni; Timothy Muzami, almaarufu ‘Timo’ ambaye alinaswa kwenye kamera za CCTV akimpiga mhasiriwa kwa mtutu wa bunduki kichwani na Hamprey Minyata, maarufu kama ‘Daddy’, 23, aliyenaswa akimtisha mhasiriwa kwa kisu.

Na wengine ni Mary Wambui, 23, ambaye alikuwa akiwaficha washukiwa nyumbani kwake katika mtaa wa Pangani na Ali Musa maarufu kama ‘Ally’ mwenye umri wa miaka 26 aliyenaswa wakati wa operesheni hiyo na anayeaminika kuwa mshirika wa wahalifu hao.

“Wanne hao walikamatwa katika maficho yao katika mitaa ya Kawangware, Gatina na Pangani. Wapelelezi walipata bidhaa mbalimbali kama vile visu, jaketi ambalo lilivaliwa na mshukiwa mmoja wakati wa wizi huo na viatu,” DCI imesema kupitia akaunti yake ya Twitter.

Taarifa ikaeleza zaidi: “Mwanamke ambaye alikuwa akiwaficha wahalifu hao nyumbani kwake Pangani na Ali Muda mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikamatwa wakati wa operesheni hiyo nao wanaaminika kuwa washirika wa wahalifu hao.”

Simu ya kisasa na kipakatalisha aina ya MacBook ambayo ni mali ya mwathiriwa pia ni miongoni mwa vitu vilivyopatikana.

Wakati wa wizi huo wa kimabavu uliotekelezwa majira ya asubuhi, wahalifu hao walionekana kwenye video wakimkaribia mwanamume huyo ambaye alikuwa amebeba begi.

Mhalifu mmoja anaonekana akimtisha kwa kisu kabla ya mwenzake kumgonga kicha kwa mtutu wa bastola.

Kisha wanampoka simu na begi yake na wanatoweka katika kichochoro fulani cha karibu.

Video hiyo ilizungushwa mitandaoni kwa kasi hali iliyofanya Wakenya kuitaka DCI kuanzisha uchunguzi wa haraka na kuwakamata wahalifu hao.

You can share this post!

Karua sasa amlaumu Uhuru

Viongozi wa kidini wataka fursa ya kutakasa shule dhidi ya...

adminleo