Habari Mseto

Yaibuka polisi huuzia watoto bangi

October 29th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA MWANGI MUIRURI

Mbunge wa Maragua Mary  Waithira amefichua magari ya polisi yanatumika kusafirisha madawa ya kulevya kaunyi ya Murang’a.

“Nimelalamikia maneno hayo  kwa kamati ya usalama ya kaunti kuhusu magari ya polisi kutumika kusafirisha dawa za kulevya.

“Niliwapa habari kuhusiana na gari la polisi ambalo limekuwa likisambazia wanafunzi wa vyuo vikuu na watoto wa chini ya miaka 18 eneo la Makuyu dawa za kulevya,” alisema.

Alisema kwamba kuna gari moja la polisi linatumika kusambaza bangi karibu na chuo cha kufunza walimu cha Murang’a na mji wa Ciumbu.

Mbunge huyo alisema kwamba abulensi na magari yanayomilikiwa na watu waliomamlakani yanatumika kwenye shunguli hiyo.

Kamishena wa kaunti ya Murang’a  Mohamed  Barre alisema kwamba anafahamu madai ya mbunge huyo. Ametupasha habari hizo na tunafanya uchunguzi. Kuna ripoti kwamba kuna maeneo ya Kabati kaunti ndogo ya Kandara kuna bohari la bangi ambalo hulindwa na polisi. Kuna vitendo vya uhalifu ambavyo huendelezwa na polisi na tunachunguza visa hivyo,” alisema.

Naibu Inspekta wa polisi Edward Mbungua aliandaa Mkutano wa usalama na wakuu wa kaungti ambapo mbunge huyo alitoa madai yayo hayo. Bw Mbungua alimpa Kamishena wa kaunti Josphat Kinyua hadi Jumatatu ashughulikie madai hayo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA