Habari za Kitaifa
Dereva wa teksi Victoria Mumbua apatikana amefariki, familia yathibitisha
DEREVA wa teksi Victoria Mumbua, ambaye alitoweka wiki moja iliyopita baada ya kusafirisha mteja kutoka Mombasa hadi Samburu, Kwale, amepatikana amefariki katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City.
Familia yake imethibitisha kwamba mwili uliopo katika mochari hiyo ni wake.
“Ni yeye,” akasema Mechack Kingi, kakake Mumbua.
“Aliokotwa kutoka Mai Mahiu.”
“Tunashuku alinyongwa na mwili wake kutupwa Ijumaa iliyopita, na kuletwa katika City Mortuary na kunakiliwa kama wa mtu asiyefahamika.”
Bw Kingi anasema kwamba sasa wanasubiri ripoti ya upasuaji.