Habari za Kitaifa

Hatma ya walimu 46, 000 wa JSS mikononi mwa Ruto, Kuppet na Knut ikiwaruka Kipetero

Na DAVID MUCHUNGUH September 6th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

HATIMA ya walimu 46,000 wa Sekondari Msingi (JSS) ambao wameajiriwa kwa kandarasi imo mikononi mwa Rais William Ruto baada yao kuachwa katika makubaliano ya kurudi kazini kati ya Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) na chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na vyuo vya kadri Kenya (Kuppet).

Walimu hao vibarua sasa wanalaumu Kuppet na chama cha kitaifa cha walimu wa shule za msingi Kenya (Knut) kwa kuwatumia na kuwatupa baada ya kutimiza matakwa yao.

Knut ilifuta mgomo mkesha wa siku uliopaswa kuanza huku wanachama wa Kuppet wakimaliza mgomo wao wa wiki moja Jumatatu jioni.

Katika mahojiano na Taifa Dijitali, Katibu mkuu wa Kuppet Akello Misori alisema suala la kuajiri walimu hao kazi ya kudumu na pensheni ni la kisiasa na chama kitazungumza na Rais Ruto.