Habari za Kitaifa

Ruto afurahia kasi ya ujenzi Talanta City

Na CECIL ODONGO April 11th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

RAIS William Ruto ameonyesha kuridhishwa na hatua ambazo zimepigwa katika ujenzi wa uga wa Talanta Sports City, mtaani Lang’ata, Nairobi.

Uga huo utasitiri mashabiki 60,000 wa soka.

Ijumaa, Aprili 11, 2025, Rais alisema wafanyakazi 3,000 ambao wameajiriwa uwanjani humo wamekuwa wakichapa kazi nzuri ambapo, 2000 huwajibika mchana kisha 1,300 hufanya kazi usiku.

Kutokana na jinsi kasi ya ujenzi inavyoendelea, Rais alisema uwanja huo utakuwa tayari kufikia Desemba mwaka huu, 2025, jinsi ambavyo serikali ilikuwa imepanga.

Rais alifichua kuwa zaidi ya Wakenya 250,000 wameajiriwa kupitia mipango ya kuimarisha miundomsingi, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na pia masoko yanayojengwa na serikali kuu katika kaunti mbalimbali nchini.