Habari za Kitaifa
Shakahola: Korti yaagiza washukiwa wapewe taarifa za ushahidi
NA BRIAN OCHARO
MAHAKAMA ya Mombasa imeagiza kuwa, washukiwa katika kesi ya vifo vya Shakahola wapewe arafa za ushahidi utakaotumiwa mahakamani kuhusu makosa ya kuwafanyia kuwatesa watoto na kuwafanyia ukatili.
Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie, na wengine 38 ambao ni wazazi wa watoto waathiriwa waliokolewa kutoka msitu wa Shakahola wako kizuizini katika magereza ya Kilifi, Malindi na Shimo La Tewa baada ya kunyimwa dhamana.
Hakimu Mkuu Nelly Chepchirchir aliamua kesi hiyo itatajwa Mei 2, 2024.