HabariHabari za KauntiHabari za Kitaifa

Video inayoonyesha binti akiuawa kwa kunyongwa yazua hamaki

Na HILARY KIMUYU October 20th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

POLISI jijini Nairobi wanachunguza mauaji yanayoshukiwa ya Faruz Hussein, 21, zaidi ya wiki mbili baada ya tukio hilo kuripotiwa.

Mpenziwe anadaiwa kumnyonga kwa kutumia mto (pillow) kabla ya kurekodi tukio hilo na kutuma video kwa familia yake. Video hiyo ilipoibuka mitandaoni, ilizua ghadhabu huku Wakenya wakitaka hatua za haraka zichukuliwe.

Kwa mujibu wa familia, Hussein aliuawa baada ya mzozo wa nyumbani. Jamaa zake walipata habari kuhusu tukio hilo baada ya mshukiwa kuwatumia video hizo.

Familia hiyo pia inadai kuwa mshukiwa alitishia kumuua dadake mdogo Hussein, mama yao na kaka yake mwenye umri wa miaka 15, akionya kuwa angeangamiza familia nzima.

Familia iliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Sunton, Kasarani, Kaunti ya Nairobi, Septemba 30, 2026, chini ya nambari ya OB 37.