80% ya mapadre wa Vatican ni mashoga – Ripoti
MASHIRIKA Na PETER MBURU
MAPADRE wanne kati ya kila kikundi cha watano Jijini Vatican ambapo ni makao makuu ya kanisa Katoliki ni mashoga. Hii ni kulingana na kitabu kipya cha upekuzi, ambacho kitachapishwa wiki hii.
Kitabu hicho cha kurasa 570 kinachoitwa ‘In the Closet of the Vatican’ ambacho kimeandikwa na mwanahabari kutoka Ufaransa Frederic Martel kinasema kuwa baadhi ya mapadre wana mahusiano ya mbali na wanawake, huku wengine wakijihusisha katika mapenzi ya jinsia moja na kutafuta huduma za mahawara wanaume.
Baada ya kufanya mahojiano na watu 1500, mwanahabari huyo alibaini kuwa kadri mapadre walionyesha kutofurahishwa na wanaume wa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, uwezekano ulikuwa mkubwa kuwa alikuwa akishiriki ushoga.
Kitabu hicho aidha kimenakili habari za kuhofisha kuhusu visa vya ufisadi na ubinafsi huko Vatican. Kimetoboa masuala kuhusu madharau dhidi ya wanawake na mipango dhidi ya Papa Francis.
Kitabu hicho kitazinduliwa katika lugha nane na mataifa 20 Jumatano, siku ambayo Papa Francis atakuwa na kikao na mabishopu Vatican, kuhusu dhuluma za kingono.
Martel, ambaye pia ni shoga alihoji makadinali 41, mabishopu 52 na zaidi ya mapadre 200 alipokuwa akifanya utafiti wa kitabu hicho.